Matthew 22:15-20

15 aNdipo Mafarisayo wakatoka nje wakaandaa mpango wa kumtega Isa katika maneno yake. 16 bWakatuma wanafunzi wao kwake pamoja na Maherode. Nao wakasema, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu na unafundisha njia ya Mungu katika kweli bila kuyumbishwa na mtu wala kuonyesha upendeleo. 17 cTuambie basi, wewe unaonaje? Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

18Lakini Isa, akijua makusudi yao mabaya, akawaambia, “Enyi wanafiki, kwa nini mnajaribu kunitega? 19Nionyesheni hiyo sarafu inayotumika kwa kulipia kodi.” Wakamletea dinari. 20Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?”

Copyright information for SwhKC